MAFANIKIO SEKTA YA AFYA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SUMBAWANGA - RUKWA
Автор: Wizara ya Afya Tanzania
Загружено: 2025-10-20
Просмотров: 89
RUKWA – SUMBAWANGA
Katika kipindi cha miaka minne, Hospitali ya Rufaa ya mkoa Sumbawanga imekuwa mfano halisi wa mabadiliko ya sekta ya afya nchini.
Uwekezaji uliofanyika umeibadilisha taswira ya hospitali hii kuwa eneo muhimu la huduma bora zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Leo, Sumbawanga RRH inasimama imara ikiwa na miundombinu ya kisasa, vifaa tiba vya kiwango cha juu, huduma za kibingwa na ubingwa bobezi, pamoja na upatikanaji wa dawa na vipimo kwa wakati. Mageuzi haya yamepunguza muda wa matibabu na kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi wanaohudumiwa katika mazingira salama, rafiki na yenye utu.
Serikali imeendelea kuimarisha nguvu kazi kwa kuajiri watumishi wapya wa afya, hatua inayolenga kuhakikisha kila mgonjwa anapata huduma stahiki kwa kumjali na upendo.
Kupitia uongozi madhubuti wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Sumbawanga imejengeka kama ngome ya matumaini, ubunifu, na tiba bora kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa na maeneo jirani.
Makala hii maalum kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Afya, imekusanya mahojiano na mitazamo ya wananchi juu ya huduma bora wanazozipata Sumbawanga RRH ikieleza safari ya mafanikio yake katika kuinua ubora wa huduma za afya nchini.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: