🔴 MWENDO KASI WATAJWA CHANZO CHA AJALI ILIYOUA SITA RUVUMA
Автор: RUVUMA TV
Загружено: 2024-12-28
Просмотров: 4793
Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limetoa ufafanunuzi kufuatia ajali ya Gari aina ya Toyota Prado lenye Namba za usajili T 647 CVR iliyotokea baada ya Gari hilo kupinduka na kuwaka Moto na kusababisha vifo vya watu sita ambao walikuwepo ndani ya Gari Hilo.
Akizungumza na Vyombo vya Habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Marco Chilya-SACP amesema kuwa,chanzo cha ajili hiyo ni mwendokasi wa Dereva wa Gari hiyo kuikosa kona na kupelekea kugonga mwamba wa jiwe uliopo pembezoni mwa barabara hiyo ya mbinga-Nyasa ,Kisha kupinduka na kuwaka moto .
" Disemba 28, 2024 majira ya Saa 1:10 asubuhi katika kijiji cha Buruma kata ya mpapa wilaya ya mbinga mkoa wa Ruvuma, katika barabara ya mbinga -Nyasa ,Gari hiyo ambayo ilikuwa ikiendeshwa na Vicent milinga ambaye ndiye mmiliki wa Gari hilo, ambalo lilikuwa likitokea kijiji cha lumala na kuelekea Wilaya ya Nyasa liliacha Njia na kugonga mwamba wa jiwe uliopo pembezoni mwa barabara hiyo kisha kupinduka kisha kuwaka moto na kusababisha vifo vya abiria sita walikuwepo katika Gari hilo ambao walikuwa wakielekea Wilayani Nyasa kwa ajili ya kuhudhuria semina ya BVR."
Halikadharika kamanda Chilya ameorodhesha majina ya abiria waliokuwepo katika ajali hiyo ambao ni,
1.Vicent milinga-Dereva wa Gari na ndiye Mmiliki wa Gari na mkazi wa Lumala .
2.Damas Nambombe-Mwalimu wa Shule ya msingi lumala Wilayani Nyasa.
3.Dominick Albert Ndau -Mwalimu wa Shule ya msingi lumala Wilayani Nyasa.
4.Judithi Joseph Nyoni-Mwalimu wa Shule ya Msingi lumala Wilayani Nyasa.
5.John Silvester Mtuhi -Mwalimu wa Shule ya msingi lumala Wilayani Nyasa .
6.Boniphace Bosco Makupnda- mhitimu wa kidato cha sita mkazi wa kijiji cha lumala,naye alipata nafasi ya kwenda kushiriki katika mafunzo hayo ya BVR.
Miili ya Marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga kwa ajili kukamilisha uchunguzi wa kisayansi ili ndugu waweze kutambua ndugu zao.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: