MIILI MIWILI YA MASHABIKI WA YANGA IMEPATIKANA ZIWANI
Автор: LIVING WATER PLUS
Загружено: 2024-08-08
Просмотров: 30
Miili ya watu wawili waliozama maji ndani ya Ziwa Victoria wakati wakitoka Kisiwa cha Yozu kusheherekea ‘Yanga Day’ kuelekea Kitongoji cha Itabagumba, Kata ya Burihaeke wilayani Sengerema imeopolewa.
Miili hiyo ni miongoni mwa watu watano waliokuwa wakitafutwa baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria uliokuwa na watu 23 kuzama maji.
Hata hivyo, watu 17 waliokolewa wakiwa hai, huku mkazi wa Mbugani, Khadija Badru (26) akitolewa majini akiwa amefariki dunia.
Watu hao walizama Agosti 5, 2024 saa 2:00 usiku wakitoka kusheherekea na kuadhimisha Siku ya Wananchi ya Klabu ya Yanga.
Taarifa ya Polisi mkoani Mwanza Jumatano Agosti 7, 2024 imesema miili hiyo imeopolewa saa 5:00 asubuhi eneo la Butala kisiwani humo.
Waliopolewa ni Mashauri Ishabakaki (42) mkazi wa Mbugani na Jonathan Mutasyoba (50) mkazi wa Kanyara wilayani Sengerema imekabidhiwa kwa ndugu kuendelea na taratibu za mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: