Chiwelesa avunja mbavu "Sisi watu wa kagera tunasafiri maranyingi na ndege, mnatusababishia adha"
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2024-05-06
Просмотров: 987
Mbunge wa Biharamulo Magharibi (CCM), Ezra Chiwelesa amejikuta akiwavunja mbavu wabunge baada ya kusema watu wa mkoa wa kagera wanasafiri sana kwa ndege hivyo kkukosekana kwa safari nyingi za ndege kuelekea Bukoba kunawaletea adha.
Chiwelesa ameyasema hayo leo Jumatatu, Mei 6, 2024 wakati akichangia mjadala wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo ameeleza kuwa kwa sasa kusafiri kwa ndege kwenda mkoani Kagera imekuwa kama anasa kutokana na ndege moja pekee kuwa ndio inafanya safari za kwenda Bukoba.
Aidha Chiwelesa ameomba ujengwe uwanja wa Mkajunguti ili mkuwezesha ndege nyingi kwenda kwenye mkoa wa Kagera.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: