Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
dTub
Скачать

AHADI YA MWENDOKASI MBAGALA YAKWAMA TENA, SABABU ZAWEKWA WAZI

Автор: Mwananchi Digital

Загружено: 2025-09-01

Просмотров: 7547

Описание:

Huduma ya mabasi yaendayo haraka (mwendokasi) katika barabara ya Mbagala, ambayo awali ilitarajiwa kuanza leo Jumatatu Septemba mosi, 2025, imesogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa miundombinu muhimu yakiwamo mageti janja na kituo cha kujazia gesi.
Akizungumza leo Jumatatu, Septemba mosi 2025 na Mwananchi, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Dk Athuman Kihamia, amesema kuchelewa kuanza kwa huduma hiyo kunatokana na changamoto hizo, licha ya mabasi kuwa tayari yamewasili.
"Mabasi yamewasili, lakini hatutaweza kuanza kutoa huduma leo kama tulivyoahidi kwa kuwa baadhi ya miundombinu haijakamilika. Mageti janja kwa ajili ya ukataji wa tiketi bado hayajafungwa na kituo cha kujazia gesi kilichopo kwenye karakana ya Mbagala nacho hakijakamilika.
"Hata hivyo, taarifa rasmi kuhusu maendeleo ya ujenzi huo tutaitoa baada ya wiki moja,” amesema Dk Kihamia.
Mabasi hayo 151 yaliwasili katika karakana ya Mbagala Rangi Tatu usiku wa Agosti 29, 2025, baada ya kutoka bandarani, shughuli iliyochukua takribani siku mbili.
Kampuni ya wazawa ya Mofat ndiyo iliyopewa jukumu la kuendesha awamu ya kwanza ya mradi huo na imekabidhiwa kuleta mabasi 255 kati ya 755 yanayohitajika kwa mradi mzima.
Awali, wiki iliyopita, Dk Kihamia aliliambia gazeti The Citizen kwamba huduma ingeanza rasmi Septemba mosi, 2025.
Pia, Agosti 13, 2025, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipokagua miundombinu hiyo aliagiza sehemu zilizobaki zikamilishwe ili huduma ianze ndani ya mwezi huo.
Hata hivyo, wakati Majaliwa akiagiza hayo, moja ya changamoto iliyokuwa imebakia ni ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Kamata, ambacho bado hakijakamilika.
Mbali na changamoto za barabara, vituo vya mwendokasi navyo havikuwa na mageti janja kwa ajili ya mfumo wa kulipia kwa kadi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mofat, Muhammad Abdallah Kassim, akizungumza na Mwananchi wakati wakipokea mabasi hayo, alisema hawatapokea fedha taslimu kwa malipo ya nauli na badala yake abiria wanapaswa kutumia kadi za Dart au za benki ambazo tayari zitafanya kazi na mfumo huo.

"Sisi hatupokei fedha taslimu. Abiria ataweka fedha kwenye kadi na kisha atatumia kusafiri. Mageti tayari yamewasili na kazi ya kuyafunga katika vituo mbalimbali inaendelea," alisema Kassim.
Hata hivyo, ucheleweshaji huo umewavunja moyo baadhi ya wakazi wa Mbagala, akiwamo Deogratius Kisinde, aliyesema, “Tumemsikia mara kadhaa Mkurugenzi wa Dart akiahidi huduma ingeanza leo, lakini hakuna kinachoendelea. Mabasi tumeona yakiingizwa kwenye karakana tangu juzi. Ni vema mamlaka ziwe zinatoa ahadi za kitaalamu na si za kisiasa."
Mabasi hayo yenye urefu wa mita 18, yatakayobeba abiria 160 kila moja, yanatarajiwa kusafirisha kati ya abiria 325,000 hadi 400,000 kwa siku mara huduma itakapoanza.
Safari zitakuwa zikifanyika kutoka Mbagala hadi Gerezani, Kivukoni na Morocco, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

AHADI YA MWENDOKASI MBAGALA YAKWAMA  TENA, SABABU ZAWEKWA WAZI

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео mp4

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио mp3

Похожие видео

ЭТО СТОИМОСТЬ ПРОЕЗДА НА СКОРОСТНЫХ АВТОБУСАХ ДО МГБАЛЫ, ПОЧТЫ И ТЮРЬМЫ. WI-FI ЗАКРЫТ, АВТОБУС РА...

ЭТО СТОИМОСТЬ ПРОЕЗДА НА СКОРОСТНЫХ АВТОБУСАХ ДО МГБАЛЫ, ПОЧТЫ И ТЮРЬМЫ. WI-FI ЗАКРЫТ, АВТОБУС РА...

DART YAJIPANGA KUINGIA KATIKA MAJIJI MENGINE, MCHENGERWA AZINDUA KADI MPYA YA MABASI YA MWENDOKASI

DART YAJIPANGA KUINGIA KATIKA MAJIJI MENGINE, MCHENGERWA AZINDUA KADI MPYA YA MABASI YA MWENDOKASI

MTANZANIA APEWA MKATABA MIAKA 12 KUENDESHA MRADI MWENDOKASI GEREZANI - MBAGALA “MABASI 255, BIL.170+

MTANZANIA APEWA MKATABA MIAKA 12 KUENDESHA MRADI MWENDOKASI GEREZANI - MBAGALA “MABASI 255, BIL.170+

Внутри новых экологичных автобусов скоростного автобусного сообщения на сжатом природном газе в Д...

Внутри новых экологичных автобусов скоростного автобусного сообщения на сжатом природном газе в Д...

BASI LINALOTOKA TANZANIA HADI SOUTH AFRICA, NAULI LAKI 3 NA NUSU, SAFARI SIKU 3 “MMILIKI MTANZANIA”

BASI LINALOTOKA TANZANIA HADI SOUTH AFRICA, NAULI LAKI 3 NA NUSU, SAFARI SIKU 3 “MMILIKI MTANZANIA”

🔴#LIVE: WAKILI DKT. NSHALA ANAFUNGUKA MAPITO ALIYOPITIA,AGUSIA SAKATA LA LISSU....

🔴#LIVE: WAKILI DKT. NSHALA ANAFUNGUKA MAPITO ALIYOPITIA,AGUSIA SAKATA LA LISSU....

KUPPET yataka polisi kuchunguza kupotea kwa mtoto Mombasa

KUPPET yataka polisi kuchunguza kupotea kwa mtoto Mombasa

Индийская рупия снова достигла рекордно низкого уровня на фоне американских тарифов | Vantage Wit...

Индийская рупия снова достигла рекордно низкого уровня на фоне американских тарифов | Vantage Wit...

Ujio wa Mwendokasi Mbagala kulinda ajira za Makondakta na Madereva wa daladala.

Ujio wa Mwendokasi Mbagala kulinda ajira za Makondakta na Madereva wa daladala.

SHUHUDIA UZURI WA GARI ZA MWENDOKASI, CAMERA  KIYOYOZI VIMO

SHUHUDIA UZURI WA GARI ZA MWENDOKASI, CAMERA KIYOYOZI VIMO

Mwendokasi Mbagala kimeeleweka!

Mwendokasi Mbagala kimeeleweka!

В Калькутте разразилась настоящая «мессианская лихорадка» в преддверии тура величайших игроков вс...

В Калькутте разразилась настоящая «мессианская лихорадка» в преддверии тура величайших игроков вс...

Трамп представил золотую карту Visa на 1 миллион долларов | Vantage With Palki Sharma

Трамп представил золотую карту Visa на 1 миллион долларов | Vantage With Palki Sharma

Как отходы сахарного тростника могут заменить бетон

Как отходы сахарного тростника могут заменить бетон

Mabasi ya Mwendokasi zaidi ya 750 kuhudumia Mbagala

Mabasi ya Mwendokasi zaidi ya 750 kuhudumia Mbagala

‘Unahamishwa Kama Kuku’: Wananchi Hawa wa Mbagala Walalamikia Tangazo la Kuondoka Kwenye Makazi Yao

‘Unahamishwa Kama Kuku’: Wananchi Hawa wa Mbagala Walalamikia Tangazo la Kuondoka Kwenye Makazi Yao

Diamond Platnumz will be shocked when he visits MBAGALA again in 2024! Mbagala has Changed

Diamond Platnumz will be shocked when he visits MBAGALA again in 2024! Mbagala has Changed

Россияне БРЕДЯТ о победе! Ответы ОШАРАШИЛИ! Казахи ШЛЮТ Путина за кораблем! | Палата №200

Россияне БРЕДЯТ о победе! Ответы ОШАРАШИЛИ! Казахи ШЛЮТ Путина за кораблем! | Палата №200

😮Патриарх Кирилл сказал это прямо в лицо РОССИЯНАМ. Смотрите, пошёл в разнос! @Popularpolitics

😮Патриарх Кирилл сказал это прямо в лицо РОССИЯНАМ. Смотрите, пошёл в разнос! @Popularpolitics

Страна, которая притворяется бедной

Страна, которая притворяется бедной

© 2025 dtub. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]