MAMA ATELEKEZA KICHANGA CHA SIKU 3 NYUMBA YA KULALA WAGENI- NZENGA
Автор: Cg Online Tv
Загружено: 2026-01-19
Просмотров: 100
Mwanamke mmoja ambaye bado hajafahamika ametekeleza kichanga cha siku tatu katika moja ya nyumba za wageni wilayani Nzega, mkoani Tabora, kisha kutoweka kusikojulikana.
Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bi. Naitapwaki Tukai, ametoa wito kwa mzazi wa mtoto huyo kujitokeza na kujisalimisha, huku akitangaza zawadi ya shilingi laki tano kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kumpata mama huyo, ili haki ya mtoto kunyonyeshwa na kulelewa na mama yake itimizwe.
Bi. Tukai ameeleza kuwa Serikali haina nia ya kumchukulia hatua za kisheria mzazi huyo, bali inalenga kushirikiana naye katika malezi ya mtoto endapo itabainika kuwa mama huyo anaishi katika mazingira magumu ya kimaisha.
Aidha, amewasihi wananchi wa Wilaya ya Nzega kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama na Serikali, ili kuokoa maisha ya kichanga hicho ambacho kwa sasa kinahitaji upendo, ulinzi na uangalizi wa karibu kutoka kwa mzazi wake.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: