#LIVE
Автор: TANZANIA HABARI - TH TV
Загружено: 2025-12-11
Просмотров: 267
#ikulu #raissamia #uvccmtaifa #ccmtaifa #ikuluzanzibar #wazirimkuu #tanzaniahabari #thtv #wizarayamamboyandani #wizarayaujenzi #wizarayaelimu #tamisemi #bungelatanzania #bungedodoma #rcmwanza #uvccm #uvccmmwanza
Wizara ya ujenzi nchini, imemuagiza mkandarasi anayejenga daraja la Mkuyuni na barabara mbili za njia nne wilayani Nyamagana jijini Mwanza Kampuni ya Jasco, kukamilisha ujenzi huo Januari mwakani, ili kuepusha adha ya mafuriko ya kila mara na usafiri inayowakabili wakazi wa jiji hilo.
Mvua zinaponyesha, wananchi wa maeneo hayo hujikuta wakipata hasara kubwa ya upotevuwa wa mali, kushindwa kufanya shughuli zao za kibiashara na kubomokewa makazi kutokana na mafuriko, yanayosababishwa na mvua hizo zinazonyesha kila msimu wa mwaka.
Abdallah Ulega, ni Waziri wa ujenzi anayefika katika eneo hili kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, uliofikia asilimia 75% na kuigharimu serikali zaidi ya shilingi bilioni tano.
Baada ya maelekezo hayo kutolewa, Meneja wa Kampuni ya Jasco inayotekeleza mradi huo SunDeep Bach, ameahidi kuwa watakamilisha mradi wa daraja hilo kwa wakati.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: