UCHAMBUZI | Yanayojiri Iran pamoja na mvutano wa Marekani na Denmark kuhusu Greenland
Автор: UTV Tanzania
Загружено: 2026-01-21
Просмотров: 4113
Mvutano kati ya Marekani na Denmark kuhusu kisiwa cha Greenland unaendelea kuibua mjadala wa kimataifa, baada ya Marekani kuonyesha nia ya kudhibiti kisiwa hicho kwa misingi ya maslahi ya kiusalama na kimkakati. Denmark, ikishirikiana na washirika wa Ulaya na NATO, imesisitiza kuwa Greenland ni eneo lake halali, hatua inayoongeza hofu ya kuyumba kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na washirika wake wa jadi.
Wakati huohuo, nchini Iran hali ya kisiasa na kiusalama bado ni tete kutokana na shinikizo la kiuchumi, maandamano ya wananchi na mvutano unaoendelea na mataifa ya Magharibi. Hatua kali za vyombo vya usalama dhidi ya waandamanaji zimeongeza ukosoaji wa kimataifa, huku hatma ya mazungumzo ya nyuklia na usalama wa kikanda ikiendelea kuwa kitendawili.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: