RAIS MWINYI NA MRADI WA UMEME ZANZIBAR
Автор: Tifu Tv
Загружено: 2025-10-01
Просмотров: 1875
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendeleza Miradi mbalimbali ya kimkakati katika Sekta ya Nishati ili kuifanya Zanzibar kuwa na Umeme wa Uhakika.
Ameeleza kuwa Hatua hiyo kwa kiasi kikubwa itachochea kasi ya Ukuaji wa Uchumi ,Huduma bora za Umeme kwa Wananchi na Upatikanaji wa Umeme wa Uhakika katika maeneo ya Uwekezaji.
Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo alipouzindua Mradi wa Uboreshaji wa Mfumo wa Umeme Zanzibar hafla iliofanyika Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Dkt, Mwinyi amesema Uzinduzi huo ni Ishara na nia njema ya Serikali ya Utekelezaji wa Ahadi zake kwa Wananchi na kuondosha Changamoto ya kukatika kwa Umeme na Umeme mdogo katika maeneo mbalimbali na kupunguza gharama za Uendeshaji.
Aidha amesema Serikali itachukua hatua za makusudi za Ujenzi wa Miundombinu mengine mipya ikiwemo Umeme wa Jua na Upepo pamoja na mitambo ya kusambaza Umeme kwa Wananchi ikiwa lengo ni kuhakikisha takriban Wananchi 70,000 wanafikiwa na Nishati hiyo.
Rais Dkt, Mwinyi amewahakikishia Wananchi kuwa katika muda mfupi Ujao gharama za Kuunganisha Umeme Majumbani itakuwa Shilingi 100,000 badala ya Shilingi 200,000 za sasa.
Rais Dķt, Mwinyi ameeleza mikakati mengine kuwa kuviunganisha na Nishati ya Umeme Visiwa Vidogo vidogo vya Njau na Kokota pamoja na kukamilisha Mradi mkubwa wa Nyaya za Umeme wa Chini ya Bahari kwa ajili ya Kisiwa cha Pemba.
Rais Dķt Mwinyi ameipongeza Wizara ya Maji ,Nishati na Madini na Kampuni ya NOVASIS INTERNATIONAL kwa Usimamizi mzuri na kukamilisha Mradi huo kwa wakati na kutoa wito wa kutunzwa kwa mradi huo ili ulete tija na kusimamia miradi mengine ili ikamilike kwa wakati.
Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini Joseph Kilangi amesema Mradi huo uliogharimu Dola za Marekani Milioni 8.4. ambao kukamilika kwake kumeiwezesha Zanzibar sasa kupokea Umeme kutoka Tanzania Bara wa kiwango cha 132 KV kutoka 114 KV iliokuwa ikipokea awali.
Akitoa Taarifa ya Kitaalamu Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme ( ZECO) Nd,Haji Haji amesema Mradi huo ni miongoni mwa miradi ya Kimkakati ya Shirika hilo unaoongeza thamani ya huduma ya Umeme na kuchochea Kasi ya Ukuaji wa Uchumi pia Utapunguza Upotevu wa Umeme na kumaliza Tatizo la Umeme katika Maeneo ya Uwekezaji.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: