NAIBU WAZIRI DANIEL SILLO AFUNGUA MKUTANO WA VIWANDA NA MASHIRIKA YA KIJESHI AFRIKA MASHARIKI
Автор: Ulinzi Channel
Загружено: 2025-02-25
Просмотров: 243
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe Daniel Sillo, tarehe 25 Februari 2025 jijini Dar es Salaam amefungua Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Mashirika na Viwanda vya Kijeshi vya Afrika Mashariki.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, aliyekuwa Mgeni rasmi katika Mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe Dkt Stergomena Lawrence Tax aliwataka washiriki wa mkutano huo kutumia fursa ya kikao hicho muhimu cha Kimkakati katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili fursa zilizopo na kuendana na wakati uliopo wa Teknolojia ya sasa katika uhawilishaji Viwanda na Mashirika ya Kijeshi.
Aidha Mhe. Daniel Sillo ametoa rai kwa Watendaji Wakuu hao wa Viwanda na Mashirika ya Kijeshi na washiriki wa mkutano huo kujadiliana uwepo wa Viwanda na Mashirika hayo utakavyoweza kuzinufaisha nchi wanachama wa Jumuiya katika kuleta maendeleo ya kiuchumi katika nchi husika. Naibu Waziri Sillo akawakumbusha wajumbe wa Mkutano huo kuwa msingi Mkuu wa mpango wa Ushirikiano katika masuala ya Ulinzi na Usalama wa Jumuiya umetokana na lengo la msingi kuhakikisha Jumuiya ipo salama kwa kushirikiana katika masuala ya Ustawi na Maendeleo ya kiuchumi nchi wanachama hivyo akawataka washiriki wa Mkutano huo kutumia fursa ya maonesho ya masoko ya bidhaa hizo kuwanufaisha.
Mkutano wa Kimkakati wa Viwanda vya Kijeshi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki umehudhuriwa na viongozi wa Viwanda na Mashirika ya Kijeshi toka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan Kusini na Somalia.
#wizarayaulinzi #jwtz #jkt
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: