*NYUMBA ZAIDI 200 KUBOMOLEWA TANGA*
Автор: MWAMBELA TV
Загружено: 2019-09-09
Просмотров: 976
Mamlaka ya viwanja vya ndege mkoa wa Tanga imetoa siku saba za kuondoka kwa wananchi waliovamia eneo la kiwanja cha ndege na kuweka makazi yao ya kudumu kwa zaidi ya miaka kumi sasa licha ya kutolewa kwa taarifa za awali za kuondoka tangu mwaka 2017.
Akizungumza na mwambela Tv meneja wa kiwanja cha ndege mkoa wa Tanga MUSSA MCHOLLA amesema hatua hiyo imefikia baada ya mamlaka ya viwanja vya ndege mkoa wa Tanga kushinda kesi ya msingi dhidi ya wananchi hao iliokuwa ikisikilizwa na mahakama kuu ya mkoa wa Tanga.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: