RUWASA ITILIMA YAKABIDHIWA GARI, PIKIPIKI ILI KUONGEZA TIJA KATIKA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI
Автор: Taratibu Online Tv
Загружено: 2021-08-16
Просмотров: 729
Meneja wa Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira (RUWASA) Mkoa wa Simiyu Eng. Mariam Majala Leo amekadhi gari Mpya aina ya Toyota Land cruiser na PIKIPIKI aina ya TVS Uongozi wa Wilaya ya Itilima.
Akimkabidhi vitendea Kazi hivyo vitakavyo tumiwa na RUWASA Itilima kwa lengo la kuongeza tija katika utekelezaji wa miradi ya Maji Eng. Majala alisema
"Mkoa wa Simiyu umebahatika kupata gari moja tu na gari hilo ni la Wilaya ya Itilima na kwa mantiki hiyo tuna kila sababu ya kuhakikisha Wananchi waitilima wanapata maji Safi na salama ya kutosha kwani tumetoka katika asilimia 58 mpaka asilimia 73 za upatikanaji wa Maji Safi na salama, sasa tumepata na vitendea Kazi lazima tukamilishe asilimia 27 zilibakia"
Aidha, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Katibu Tawala Ndg. Filbert Kanyilizu alimshikuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea nyenzo hizi za Kazi kwa hakika hatuta muangusha.
Naye Mbunge wajimbo la Itilima Mhe. Njalu Silanga alisema
" Mpaka kufikia asilimia 73 Kuna Kazi kubwa imefanyika ingawa hatukua na usafiri wa uhakika, sasa tunaenda kuzitafuta asilimia zilizo salia"
Meneja wa RUWASA Itilima Eng. Banda ISSA aliahidi kuvifikia Vijiji vyote 102 vya Wilaya Itilima kwa huduma ya Maji Safi na salama.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: