PROFESA KABUDI ALIVYOZUNGUMZIA SUALA LA UKABILA NCHINI KENYA
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2019-11-28
Просмотров: 9025
Hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi katika uzinduzi wa Ripoti ya Jopo la Maridhiano (BBI) nchini Kenya ni mjadala kila kona.
Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kauli za watu wa kada mbalimbali katika mitandao ya kijamii kuhusu alichokisema waziri huyo.
Katika uzinduzi huo Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alitoa mapendekezo ya muundo wa Serikali unaokaribia kushabihiana na Tanzania.
Katika hotuba yake Profesa Kabudi aliwataka Wakenya kuwa na mshikamano kama wa Tanzania na kuachana na ukabila, “Kenya inapoungana, Afrika Mashariki pia inaungana."
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: