PROF SAID '''WAPENI MUDA WA NYONGEZA WATAHINIWA WENYE MAHITAJI MAALUM'''
Автор: sauti yetu TV
Загружено: 2025-11-17
Просмотров: 144
SAUTI YETU ONLINE TV,,,WORLD WIDE,,,Jumla ya watahiniwa 595,816 wameanza mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari nchini hii leo November 17 2025 hiyo ni kwamujubi wa taarifa iliotolewa na katibu mtendaji wa baraza la mitihani necta prof said Mohamed.
Akizungumza na waandishi wa habari novemba 16 Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Prof. Said Mohamed, amesema mtihani huo utafanyika kwa siku 19 kuanzia Novemba 17 hadi Desemba 5, 2025 katika jumla ya shule za sekondari 5,868 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 813.
Kati ya watahiniwa wa shule 569,914 waliosajiliwa mwaka 2025, wavulana ni 266,028 sawa na asilimia 46.68 na wasichana ni 303,886 sawa na asilimia 53.32.
Aidha, wapo watahiniwa wa shule 1,128 wenye mahitaji maalum ambapo kati yao, wenye uoni hafifu ni 860, wasioona ni 70, wenye uziwi ni 58, wenye ulemavu wa akili ni watano na wenye ulemavu wa viungo ni 135,” amesema.
Alisema kati yao, 569,914 ni watahiniwa wa shule na 25,902 ni watahiniwa wa kujitegemea.
Kwa upande wa watahiniwa wakujitegea wapo wenye mahitaji maalum 56 ambapo kati yao wenye uoni hafifu 49 na wasiiona 7
Aidha baraza la mitihani necta limeonya watakaobainika kufanya udanganyifu watafutiwa matokeo yao pamoja na kuwachukulia hatua watakaosababisha vitendo hivyo.
#wasafi #utvonline #azamtv #tbc #bbcswahili #albayaan
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: