HUMOUD JUMAA, MHANDISI NYAMO-HANGO NA MSOFE WATEMBELEA VIJIJI MIKAKATI YA UMEME
Автор: BILL MEDIA
Загружено: 2016-09-18
Просмотров: 255
HUMOUD JUMAA, MHANDISI NYAMO-HANGO NA MSOFE WATEMBELEA VIJIJI MIKAKATI YA UMEME
Na Omary Mngindo, Kibaha Pwani Tanzania Sept 18
MBUNGEwa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Tanzania Humoud Jumaa amewaongoza Wahandisi wa Wakala wa Nishati vijijini (REA) kutembelea katika vijiji vitatu jimboni humo kuzungumzia mikakati ya upatikanaji wa huduma hiyo maeneo hayo.
Mbunge Humoud aliongozana na Mhandisi Boniface Nyamo-Hanga Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Nishati vijijini (REA), Mhandisi Bengiel Msofe, Mhandisi Martine Madulu Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani na Mwakatobe Leo Mhandisi wa Miradi ya Umeme mkoani hapa.
Ziara hiyo ilianzia katika kijiji cha Mpiji kilichopo Kata ya Boko Mnemela, Kitongoji cha Kibwende Kata ya Mlandizi mjini na Kijiji cha Mwanabwito Kata ya Kikongo ambapo viongozi hao walizungunzia mikakati mbalimbali ya upatikanaji wa nishati hiyo ya umeme.
MWISHO.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: