🔵AJALI MBAYA MAKULU DODOMA BODABODA WANNE WAFARIKI DUNIA PAPO HAPO
Автор: JIMBI TV
Загружено: 2025-12-11
Просмотров: 456
AJALI MBAYA YAUA BODABODA WANNE MAKULU, DODOMA
Dodoma, Tanzania — Ajali mbaya imetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Makulu jijini Dodoma baada ya lori la mchanga kupoteza mwelekeo na kutoka barabara kuu, kisha kuelekea pembeni katika eneo ambalo bodaboda huwa wanapaki, na kuwagonga bodaboda waliokuwepo.
Katika ajali hiyo, bodaboda wanne wamefariki dunia papo hapo, huku wawili wakijeruhiwa vibaya.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Shekimweri, alifika eneo la tukio na kushuhudia hali halisi ya ajali hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa hili si tukio la kwanza kutokea katika eneo hilo kutokana na kona kali iliyopo na mwonekano mdogo wa barabara wakati wa usiku.
Ameeleza kuwa serikali itachukua hatua za dharura ili kuzuia ajali zaidi, ikiwemo:
Kuweka matuta katika eneo hilo la Makulu
Kusimika kibao cha tahadhari kinachoonyesha kuwepo kwa kona kali
Mhe. Shekimweri ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa familia za marehemu na kuwaomba madereva kuongeza umakini wanapopita katika eneo hilo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: