'FANYENI SHUGHULI MLIZOKUSUDIA-DC BUSWELU
Автор: Bugoma TV
Загружено: 2025-12-22
Просмотров: 59
KATAVI: Zaidi ya milioni 251 zimetolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni mkopo wa sehemu ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ndani ya halimashauri ya wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amesisitiza vikundi hivyo kufanya shughuli zenye tija zaidi ambapo amewata kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali ikiwemo mikopo hiyo.
Aidha amewaasa vijana kujikita katika shughuli za kilimo kwani serikali inaendelea kuboresha sekta hiyo ikiwemo kutoa pembejeo na mbegu za mazao mbalimbali ikiwemo mbegu za ufuta.
Kwa upande wake afisa maendeleo wa halimashauri hiyo Halima Kitumba amesema kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali watahakikisha wanaendelea kutoa elimu ya biashara sanjari na kuwaonesha fursa muhimu ikiwemo kilimo kwa vijana.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: