NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA MEI MOSI 2025
Автор: SKY TV
Загружено: 2025-04-15
Просмотров: 81
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuanzia Mei Mosi mwaka huu itasitisha matumizi ya namba za utambulisho kwa wale wote ambao walishatumiwa ujumbe mfupi wa maneno lakini hawakwenda kuchukua vitambulisho vyao katika ofisi za kata, vijiji, mitaa, vitongoji na shehia.
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema hadi kufikia Machi 23,2025 wananchi 1,880,608 waliokuwa hawajachukua vitambulisho wametumiwa na kupokea ujumbe mfupi wa maneno lakini waliojitokeza kuchukua ni 565,876.
Katika hatua nyingine mamlaka hiyo imesema kuanzia Julai mwaka huu itaanza kusajili watu wenye umri chini ya miaka 18 na majaribio yataanza katika Wilaya za Kusini Unguja, Kilolo, Iringa na Rungwe ambapo wanatarajia kusajili watu 235,826 ndani ya miezi miwili.
#skytv
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: