Mifupa ya binadamu imepatikana eneo la Karai, Kikuyu
Автор: Citizen TV Kenya
Загружено: 2026-01-20
Просмотров: 4454
Hali ya Wasiwasi imetanda katika Kijiji cha Karai, eneo bunge la Kikuyu, Kaunti ya Kiambu, baada ya mifupa inayokisiwa kuwa ya binadamu kupatikana katika uwanja wa Karai.
Eneo hilo lina mabwawa na vyanzo vya maji, na hutumiwa na wakazi pamoja na watu kutoka maeneo jirani, hali inayozua wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wao. Maafisa wa Polisi walifika katika eneo la tukio na kukusanya mifupa hiyo, ambayo imepelekwa katika maabara ya serikali kwa uchunguzi zaidi.
Wakazi sasa wanatoa wito kwa serikali na mamlaka husika kuhakikisha mabwawa katika eneo hilo yanawekwa vizuizi, ili kuzuia visa vya watu kutumbukia humo
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: