VIONGOZI WA DINI GEITA WATOA WITO WA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.
Автор: MwangazaTV
Загружено: 2025-10-28
Просмотров: 37
#mwangazatvupdates
Kamati ya Amani Mkoa wa Geita imetoa tamko la pamoja kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika kesho, Oktoba 29, 2025, ikihamasisha wananchi na waumini wote kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani na uhuru.
Viongozi hao wa dini wamesisitiza kuwa kushiriki uchaguzi ni wajibu wa kikatiba kwa kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura.
Akisoma tamko hilo kwa niaba ya viongozi wenzake, Askofu Reuben Ng’wala ambaye ni kiongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Geita, amesema kuwa ni muhimu kwa wananchi kutimiza haki yao ya kidemokrasia kwa utulivu na bila kushawishiwa au kuingiliwa na mtu yeyote.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: