MOTO WATEKETEZA WATOTO WAWILI KILIMANJARO
Автор: SAFARI ZETU TV
Загружено: 2025-12-17
Просмотров: 352
Akizungumza Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremia Mkomagi, amesema kuwa majira ya saa 5:11 asubuhi, Jeshi la Zimamoto lilipokea taarifa ya tukio la moto lililotokea katika nyumba ya Bw. Siza.
Alisema kuwa mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Jeshi la Zimamoto lilifika eneo la tukio na kubaini kuwa moto ulikuwa tayari umeteketeza sehemu ya nyumba, ukiwa umeanzia sebuleni.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, moto ulianza majira ya saa 4:00 asubuhi, wakati dada mmoja alipokuwa anawapatia uji watoto wawili wenye umri wa miaka 2 na 4, wote jinsia ya kiume. Baada ya kuwapatia uji, alitoka nje kusafisha vyombo, ndipo alipoona moto ukiwa tayari umesambaa katika eneo la sebule.
Aliongeza kuwa dada huyo alianza kupiga kelele kuomba msaada kutoka kwa wananchi waliokuwa jirani. Wananchi walijitokeza na kuanza juhudi za kuokoa, hata hivyo, Jeshi la Zimamoto lilipofika eneo la tukio, watoto hao walikuwa tayari wamenaswa na moto.
Kwa masikitiko makubwa, juhudi za kuwaokoa hazikufanikiwa, na watoto wawili walipoteza maisha katika tukio hilo.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha moto huo, huku likitoa pole kwa familia na ndugu wa marehemu.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: