Sijaridhika!! Hali na Kasi ya Ujenzi wa Barabara ya Wenda-Mgama (Mufindi) na Mtili-Ifwagi (Iringa)
Автор: Focus TV Tanzania
Загружено: 2024-03-30
Просмотров: 653
Naibu katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Rogatus Mativila, ameonesha kutokurishishwa na hali pamoja na kasi ya Utekelezaji wa miradi ya Ujenzi wa Barabara ya Wenda - Mgama yenye Urefu wa Km 19 katika Halmashauri ya Iringa na Barabara ya Mtili - Ifwagi - Mkuta yenye Urefu wa Km 14 katika Halmashauri ya Mufindi.
Ujenzi wa barabara hizo unetekelezwa na mkandarasi kutoka kampuni ya CHINA HENAN INTERNATIONAL COOPERATION GROUP (CHICO) kwa ghrama ya shilingi bilioni 52.72 na kusimamiwa na mtaalamu mshauri kutoka kampuni ya AFRISA CONSULTING LIMITED kwa gharama ya shilingi milioni 797.
Akisoma taalifa ya Utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa barabara hizo, Meneja wa TARURA mkoa wa Iringa, Mhandisi Tembo amesema ujenzi wa barabara ya Wenda - Mgama kwa kiwango cha lami unatekelezwa kwa muda wa miezi 18 kuanzia Julai 27, 2023 hadi Januari 27, 2025 huku akisema kuwa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 7 ambapo lengo lilikuwa ni kufikia asilimia 10.
Mhandisi Tembo, amesema Utekelezaji wa mradi huo haujawa katika kasi iliyokusudiwa hali iliyopelekea kufanya vikao mbalimbali vilivyohusisha viongozi wa juu wa pande zote za mradi (TARURA, Mtaalamu mshauri na Mkandarasi). Aidha, katika vikao hivyo ilikubaliwa kwamba hadi kufikia mwezi Juni mkandarasi awe amefikia asilimia 33 ya utekelezaji wa mradi.
Kwa upande wa ujenzi wa barabara ya Mtili - Ifwagi - Mkuta kwa kiwango cha lami, mhandisi Tembo amesema ujenzi huo unatekelezwa kwa muda wa miezi 15 kuanzia Agosti 22, 2023 hadi Novemba 22, 2024 huku akisema kuwa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 8 ambapo lengo lilikuwa ni kufikia asilimia 12.
Vile vile mhandisi Tembo, amesema utekelezaji wa mradi huo haujawa katika kasi iliyokusudiwa hali iliyopelekea kufanya vikao mbalimbali vilivyohusisha viongozi wa juu wa pande zote za mradi (TARURA, Mtaalamu mshauri na Mkandarasi). Aidha, katika vikao hivyo ilikubaliwa kwamba hadi kufikia mwezi Juni mkandarasi awe amefikia asilimia 53 ya utekelezaji wa mradi.
Mradi wa ujenzi wa barabara hizo ukikamilika utasaidia kuboresha huduma ya usafiri na usafirishaji ambapo kutapelekea kusafirisha mazao kirahisi kwenda kwenye masoko hivyo kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla, lakini pia utasaidia katika upatikanaji wa ajira kwa wananchi hasa wanaoishi katika maeno yaliyopo katibu na miradi hiyo.
Subscribe (Focus Digito TV) ili usipitwe na Video mpya zinazotoka kila siku.
Focus Digito TV inakupa Maudhui Mazuri yanayohusu Habari, Elimu, Mitindo ya maisha, Michezo na Burudani.
Focus Digito TV is here to provide you with contents about News, Education, Lifestyles, Sports and Entertainments.
#FocusDigitoTV
..................
Tufuatilie Zaidi kupitia:
INSTAGRAM, TIKTOK, FACEBOOK, TWITTER (X), THREADS NA GOOGLE WEBSITE YETU YA FOCUS DIGITO TV
Focus Digito TV is one of the best info-edu-tainment Online Media conveying contents for the Public Interest.
Asante kwa kuchagua kutufuatilia | Thanks for Subscribing
We Love You | Tunakupenda
Regards
Team FocusDigitoTV
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: