KWAYA YA UINJILISTI KIJITONYAMA | USIOGOPE
Автор: Uinjilisti Kijitonyama Choir
Загружено: 2025-03-07
Просмотров: 12569
USIOGOPE, Yesu yupo kila mahali na kila hatua ya maisha yako. Hatakuacha kamwe.
Karibu ushiriki nasi katika maneno haya ya ushindi na kutia moyo kupitia wimbo huu ulio imbwa na Kwaya Ya Uinjilisti Kijitonyama, katika ibada ya SIku ya Mbingu Kujaa Sifa msimu wa nne. (S04)
Lyrics
USIOGOPE
Chorus: Usiogope eeh ndugu, Yesu yupo mbele yako, yupo nyuma yako, kushoto kulia Yesu yupo, zaidi akufunika kwa Damu yake ya thamani, usiogope ee
Verse 1
Kamwe usije ukawaza Mungu kakuacha ee ndugu, ujapopitia majaribu mbalimbali eeh,
Mungu amekusudia kukutengenezea njia, ukishayashinda yote imani yako itakua,
kumbuka majaribu kipimo cha imani yako, usiogope..
Chorus
Verse 2.
Hata kama nyuma yako kwaja majeshi ya farao,
hata kama mbele yako kunayo bahari ya shamu,
hofu na mashaka visiutawale moyo wako e ndugu mpendwa,
maana kwa neno lake Bwana bahari itakuwa njia,
maana kwa neno lake Bwana bahari itakuwa njia
Chorus
Verse 3
Solo: Subiri yeyeye subiri kutoka kwa Yesu, subiri yeyeye, atakujibu kwa wakati, subiri yeyeye majibu kutoka kwa Yesu subiri yeyeye, utajibiwa kwa wakati eeeh
Wote: Subiri yeyeye, subiri kutoka kwa Yesu, subiri yeyeye atakujibu kwa wakati
Solo: …..free style
Wote:Subiri yeyeye, subiri kutoka kwa Yesu, subiri yeyeye atakujibu kwa wakati
Verse 4:
Yeye ni mwanzo na tena ni mwisho ahadi zake hazipimwi kwa muda,
miaka elfu kwenye hii dunia kwake Bwana sawa na siku moja X2
subiri eeh, subiri eeh, subiri eeh baba, subiri eeh, subiri eeh,
subiri eeh mama, subiri eeh, subiri eeh, subiri eeh kaka, subiri eh subiri eeh,, leleleleee
Wote: Subiri yeyeye, subiri kutoka kwa Yesu, subiri yeyeye atakujibu kwa wakati

Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: