Ujue Mfumo wa PlanRep - CCSWOP
Автор: Pact Tanzania
Загружено: 2022-01-05
Просмотров: 941
CCSWOPG ni mwongozo kabambe wa mipango, vipaumbele na bajeti za Ustawi Wa Jamii ngazi ya Halmashauri.
CCCSWOP Kama mpango unaoratibiwa Kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI unalenga yafatayo:-
1. Kuimarisha mipango na uratibu wa Shughuli za Ustawi Wa Jamii katika ngazi za Serikali za mitaa
2. Kurahisisha upatikanaji wa rasilimali kwaajili ya shughuli za Ustawi Wa Jamii
3. Kuimarisha upatikanaji wa taarifa na takwimu za kiustawi WA jamii
4. Kuboresha huduma Kwa makundi maalumu katika jamii.
Mpango WA CCSWOP umeunganishwa katika mfumo wakielekroniki wa mipango na taarifa za Serikali (PlanRep) wa Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kurahisisha upangaji, upimaji wa mipango na ufuatiliaji wa mipango na bajeti katika ngazi zote za huduma na maamuzi.
Shirika la Pact Tanzania kupitia Mradi wa ACHIEVE tumeshirikiana na Serikali katika kufanikisha zoezi la umaliziaji na urasimishwaji wa CCSWOP, na kuasisi zozezi la kuambatanisha CCSWOP katika PlanRep.
ACHIEVE pia imeendelea na utoaji mafunzo matumizi sahii CCSWOP Kwa kamati za mipango ya Ustawi Wa Jamii (Council Social welfare Planning Teams) kwenye Halmashauri 81 zinazofikiwa na mradi.
Matarajio ya ACHIEVE na Serikali ni kuona huduma na taarifa za Ustawi Wa Jamii zikiimarika na kushamiri zaidi kupitia utekezaji wa CCSWOP.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: