BABA MDOGO ATAJA CHANZO NAOMI KUUAWA NA MUMEWE, "TUTAZIKA TENA MAJIVU YAKE YALIOPANDIA MIGOMBA"
Автор: Capital Digital
Загружено: 2025-02-26
Просмотров: 619
BABA MDOGO ATAJA CHANZO NAOMI KUUAWA NA MUMEWE
#HABARI: Vilio, simanzi na majonzi vimetawala wakati Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam ilipomhukumu mfanyabiashara Khamis Luwonga (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa makusudi.
Hukumu hiyo imesomwa leo na Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama hiyo baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha shtaka hilo bila kuacha shaka lolote na huku ikieleza kwamba katika maelezo ya onyo ya mshtakiwa alichokieleza ni kweli kwamba alimuua mke wake na kisha kumchoma moto.
Hata hivyo, mshtakiwa baada ya kutiwa hatiani na mawakili wa pande zote mbili kuzungumza mshtakiwa, alitaka kuzungumza, Jaji Mwanga alikataa na kumueleza asubiri kwanza lakini alikaidi ndipo Jaji akaita askari kumtuliza ili aendelee na kutoa adhabu.
Jaji Mwanga alisema hilo ni kosa la mauaji mikono yake imefungwa kiapo chake cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sheria za Tanzania adhabu ni moja tu kunyongwa hadi kufa.
Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi Ashura Mnzava aliiomba mahakama iwapatie mabaki ya mwili wa naomi ambayo yalitolewa kama kielelezo, ambapo ndugu wameomba wakayazike mabaki hayo kwa sababu hawakuwahi kufanya mazishi ya mpendwa wao.
Baba mdogo wa marehemu, Richard Marijani akiwa nje ya mahakama alisema watakwenda kuzika mabaki hayo ili kumpuzisha ndugu yao mpendwa ambaye hakuwahi kuzikwa tangu umauti wake huku pia akitaja chanzo cha mauaji hayo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: