NDC–TZ YARIDHISHWA NA MABORESHO BANDARI YA TANGA
Автор: MWAMBELA TV
Загружено: 2026-01-19
Просмотров: 111
NDC–TZ YARIDHISHWA NA MABORESHO YA BANDARI TANGA
Imeelezwa kuwa maboresho makubwa yaliyofanywa katika Bandari ya Tanga yameleta tija katika sekta ya usafirishaji na kuchochea ukuaji wa uchumi katika mikoa ya Kaskazini na Kaskazini Mashariki mwa Tanzania pamoja na nchi jirani.
Akizungumza wakati wa ziara ya mafunzo kwa vitendo ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania (NDC–TZ), Brigedia
Jenerali Baganchwera Rutambuka amesema upanuzi wa gati na uboreshaji wa miundombinu umeongeza ufanisi wa utoaji huduma, hali iliyopelekea kuongezeka kwa idadi ya meli, shehena za mizigo, mapato ya bandari pamoja na kupungua kwa muda wa kushusha mizigo.
Brigedia Jenerali Rutambuka ameongeza kuwa Bandari ya Tanga ina nafasi ya kipekee ya kuwa kitovu muhimu cha usafirishaji kwa ukanda wa Kaskazini endapo maboresho yataendelea kufanyika, akibainisha kuwa ni bandari muhimu inayohudumia maeneo mengi ya kanda hiyo.
Comment
Like
Share
Subscribe
#MWAMBELAINFO
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: