Qaswida nzuri| Abubakar Barisa akimuimbia mke wake siku ya harusi yao🔥🔥ft Mu Zain..
Автор: ABUBAKAR BARISA 001
Загружено: 2022-11-30
Просмотров: 13957
kukushukuru Latwifu
Ni wajibu ni lazima.
Mola ndoa kaiswifu
kwa mawadda na huruma.
Rabbi tupe watwiifu
watulivu wake wema.
shairi hili la kwangu
nimelitunga kusudi.
kukusifu mke wangu
kwani hilo sina budi.
wewe ndiwe nusu yangu
kwa baraka za Wadudi.
mke ni mwenye tabia
ndivo tulivoambiwa.
amjuwae Jalia
na Tumwa wake Moliwa.
nawe nakuaminia
dini umejaaliwa.
ndiwe swabahul kheri
unaponipa salamu.
ndiwe masau nnuri
pale ukitabasamu.
mimi nawe nakariri
ni kama nyama na damu.
ninayo kubwa imani
utakuwa mtwiifu.
kisha utanithamini
na wingi uaminifu.
ndoa ipate makini
siku zote nikusifu.
Mungu atupe umuri
ulosheheni mahaba.
Atupe wana wa kheri
na wajukuu si haba.
tumswalie Bashiri
ali zake na swahaba.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: