KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - FRIDAY PRAYE 05 DECEMBER 2025
Автор: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
Загружено: 2025-12-05
Просмотров: 4015
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - FRIDAY PRAYE 05 DECEMBER 2025
SIKU YA 33 YA MAFUNGO YA KUMALIZA MWAKA 2025 NA KUOMBEA MWAKA 2026
SOMO : KUZUILIWA KUWA (MIKAKATI YA KIROHO)
Kutoka 3 : 19
Matendo 12 : 1 - 12
Daniel 9 : 22
Esta 3 : 7
Mithali 16 : 4
Esta 4 : 15 - 16
Esta 9 : 1 - 2
MADA:
"FROM HOW TO WHO"
(INAWEZEKANA)
NENO KUU:
"HOW SHALL THIS BE?"
(LITAKUWAJE NENO HILI?)
LENGO LA SOMO:
Mungu kukupa AKILI ili upate Ufahamu juu ya Vita ya KUZUILIWA KUWA na UKUBALI Mungu akuweke anavyotaka ili USHINDE na KUJALIWA KUWA.
MKAKATI WA KIROHO KUSHUGHULIKA NA MAJIRA
(MKAKATI WA KIMAJIRA)
Kutoka 3 : 19
Danieli 9 : 22
Mwanzo 8 : 22
Yoel 2 : 25
Waamuzi 16 : 22
Hesabu 25 : 1 - 3
Kutoka 3 : 19
19 Nami najua ya kuwa huyo mfalme wa Misri hatawapa ruhusa mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu.
Danieli 9 : 22
22 Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu.
Mwanzo 8 : 22
22 Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
Yoel 2 : 25
25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.
Waamuzi 16 : 22
22 Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake.
Hesabu 25 : 1 - 3
1 Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu;
2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao.
3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli.
1. Mungu pekee ndiye anayeweza KUREKEBISHA na KUREJESHA majira yaliyovurugwa na kuharibiwa katika maisha ya mtu.
2. Jizoeze Mara kwa Mara kutoa sadaka maalumu Kushughulikia MAJIRA chini ya SADAKA kuu ya Damu ya YESU.
AGENDA ZA MAOMBI FRIDAY PRAYERS
1. Kuomba TOBA kwa kuwakaribisha na Kujiungamanisha na watu Bila Maelekezo ya Mungu.
2. Omba Mungu akutenge na watu wasio sahihi KIMAJIRA
3. Omba Mungu akukutanishe na Kukuunganisha na watu sahihi katika Kila nyanja ya maisha yako.
4. Omba Mungu akupiganiye VITA ya eneo la Watu.
5. Omba Mungu arekebishe na kukurejeshea Majira yako yaliyovurugwa.
6. Ombea MAONO yako ya kumalizia 2025 na yale ya 2026
Mhubiri : Mwl. Eng Goodluck Mushi.
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : [email protected]
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: