ORYX GAS YAKABIDHI ZAWADI KWA WATEJA KAMPENI YA GESI YENTE' WAUNGA MKONO SERIKALI NISHATI SAFI
Автор: Global TV Ripota
Загружено: 2025-12-01
Просмотров: 13
Kampuni ya Oryx Gas Tanzania leo imekabidhi zawadi mbalimbali kwa wateja walioshinda kupitia kampeni yao ya GESI YENTE, ambayo inalenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba Mosi, 2025 wakati wa hafla ya utoaji zawadi, Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Shaban Fundi, alisema Oryx itaendelea kuwekeza katika miundombinu na kupanua mtandao wa usambazaji ili kusaidia utekelezaji wa ajenda ya matumizi ya nishati safi kwa afya bora, uhifadhi wa mazingira na maendeleo endelevu.
“Kama Tanzania imeweka lengo la asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034, sisi kama Oryx hatuko nyuma. Tumejipanga kuhakikisha huduma zetu zinawafikia wananchi kupitia mawakala wakubwa na wadogo,” alisema Fundi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: