NI MABILIONI | MFANYABIASHARA WA MBAO MAFINGA AKAMATWA KWA UHUJUMU UCHUMI
Автор: IPC Mkombozi TV
Загружено: 2025-09-29
Просмотров: 17692
Mfanyabiashara wa mbao kutoka Mafinga, Mosses John Madege, amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Iringa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 23655 ya mwaka 2025.
Kesi hiyo imesomwa kwa mara ya kwanza leo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Japhet Bwire Manyama.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Medalakini Emmanuel, akisaidiwa na Auni Chilamula, uliwasilisha mashtaka 25 dhidi ya mtuhumiwa huyo.
Imeelezwa mahakamani kuwa kati ya mwaka 2022 hadi 2024, mtuhumiwa alidaiwa kuwasilisha ritani za Kodi ya Ongezeko la Thamani zenye taarifa za uongo, kinyume na kifungu cha 84(1) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi. Katika ritani hizo, Madege alionyesha kuwa amefanya manunuzi kupitia mfumo wa malipo kwa taasisi za umma, maarufu kama GPG, ilhali taarifa hizo hazikuwa sahihi.
Mashtaka hayo yanajumuisha makosa 23 ya awali ya kuwasilisha taarifa za uongo, kosa la 24 la kukwepa kodi kwa njia ya udanganyifu, na kosa la 25 la uhujumu uchumi kwa kusababisha hasara kwa Mamlaka ya Mapato kutokana na kodi ambayo haikulipwa.
Madege alifikishwa mahakamani na Idara ya Upelelezi wa Kodi Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. Hata hivyo, licha ya kupewa masharti ya dhamana ikiwemo kuweka nusu ya fedha za hasara aliyosababisha, alishindwa kukidhi masharti hayo na kurejeshwa mahabusu.
Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena Oktoba Mosi, mwaka huu.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: