SAKATA la USAFIRI Kilimanjaro EXPRESS Lipo hivi!! Mkurugenzi, Mwanasheria WAFUNGUKA
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2024-01-08
Просмотров: 24609
Mkurugenzi wa mabasi ya Kilimanjaro Express, Rolent Sawaya amesema anapata maumivu kutokana na biashara zake kukwama huku akimuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kuingilia kati kumsaidia.
Kauli hiyo inakuja wakati kampuni hiyo ikisimamishwa kutoa huduma katika njia za Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha kwa kile kilichoelezwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) kuwa ni ukiukwaji wa masharti ya leseni ikiwemo kudaiwa kutotumia tiketi mtandao na kutoza nauli tofauti na iliyopangwa.
Akizungumza leo Januari 8, 2024 katika kikao kilichowakutanisha Chalamila na maofisa wa Latra kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa sakata la kampuni hiyo kuzuiwa kutoa huduma na kusababisha adha kwa abiria waliokuwa wamepanga kusafiri na mabasi ya Kilimanjaro Express.
.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: