Waziri Lugola awaonya askari 'Ole wake askari atayeongozwa na njaa zake'
Автор: Millard Ayo
Загружено: 2019-05-17
Просмотров: 5385
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi KANGI LUGOLA amelitaka jeshi la polisi mkoa wa MOROGORO kumpa maelezo ya kina juu ya askari wa jeshi la polisi wanaoda kufanya vurugu katika kiwanda cha tumbaku cha Tanzania relif tobacco kilichopo mjini MOROGORO tukio lililofanyika Dec 2018
Waziri LUGOLA ametoa agizo hilo baada ya kutembelea kiwandani hapo na kupokea malalamiko kutoka kwa mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda hicho RICHARD SINAMTWA akidai baadhi ya askari walikwenda kiwandani hapo kwa nia ya kuwakamata viongozi bila kubainisha kosa
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi KANGI LUGOLA ametembelea kiwanda cha cha tumbaku cha Tanzania relief tobacco na kupokea malalamiko dhidi ya baadhi ya askari polisi wanaodaiwa kufanya vurugu katika kiwanda hicho
Kufuatia malalamiko hayo,waziri LUGOLA akatoa maagizo kwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa MORGORO WILBROAD MUTAFUNGWA kumpelekea maagizo ya kina juu ya tukio hilo ndani ya siku moja
Aidha akawaonya askari wanaotumia vibaya nafasi zao kuwanyanyasa wanachi wasio na hatia kuacha mara moja tabia hiyo vinginevyo serikali itawachukulia hatua kali za kinidhamu
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: