Matapeli watano wanaswa Arusha, Wananchi wengi walizwa
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2023-11-23
Просмотров: 8798
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kujifanya maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kutapeli wananchi katika maeneo tofauti tofauti Mkoani humo.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Fredy Malaki (34) mkazi wa Karakata, Francis Mwita (42) mkazi wa Ukonga, Fidelis Joseph (27) mkazi wa Msumi Mbezi, Selina Fortunatus (43) makazi wa Temeke wote kutoka Jijini Dar es salaam na Fereji Hamadi (40) mkazi wa Tabora.
Aidha ACP Masejo amebainisha kuwa bado Jeshi hilo linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na pindi upelelezi utakapo kamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: