UJUMBE: PIGANA VITA VIZURI VYA IMANI || EV. EZEKIEL MPAPATO
Автор: FPCT Mlimani
Загружено: 2025-07-20
Просмотров: 39
1 Timotheo 6:12
[12]Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.
Waebrania 11:1,6
[1]Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
[6]Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Warumi 1:17
[17]Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.
★Mungu anadhihirika endapo utakuwa na Imani .
★ Kama hujapanda viwango vya kumuamini MUNGU huwezi kuona akidhihirika kwenye maisha yako.
VITA VYA IMANI VILIVYO VIZURI
★Spiritual (vita vya kiroho- KUISHI MAISHA MATAKATIFU.
Waefeso 6:12-13
[12]Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
[13]Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
★Vita vya Imani. - KUWA NA IMANI THABITI.
Mathayo 4:1-2,4
[1]Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.
[2]Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.
[4]Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
★Kufuata wito wa MUNGU
★Kushinda hofu na mashaka.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: