Wanataka baraka za Mungu, lakini hawataki Neno la Mungu.
Автор: KKKT KARIAKOO
Загружено: 2025-11-21
Просмотров: 344
“Wanataka Kukombolewa, Lakini Wabaki Babeli”
Mungu ana mpango wa furaha, amani, na uzima wa milele juu ya maisha yako. Kubali uongozi wake, na uone akibadilisha kila “michongoma” ya maisha kuwa msunobari wa baraka.
Leo tunakutana na ukweli unaoumiza kanisani na katika maisha ya waamini wengi. Watu wanatoka kukombolewa, lakini hawataki kutoka Babeli. Wanatoka Misri kimwili, lakini mioyo yao bado inatamani vitunguu vya Misri. Wanataka baraka za Mungu, lakini hawataki Neno la Mungu.
Babeli ni picha ya mfumo wa dunia, dhambi, tamaa, uzembe wa kiroho, na maisha bila utii. Wengi wanataka mkono wa Mungu, lakini hawataki uso wa Mungu. Wanataka Mungu awaponye, awainue, awafungue milango—but hawataki kubomoa madhabahu za Babeli zilizo ndani yao.
Mungu hapokei ibada ya midomo tu. Hatabariki maisha ambayo hayako tayari kutii. Baraka za Mungu haziwezi kudumu kwa mtu ambaye hajakubali kubadilishwa na Neno la Mungu.
Kumbuka:
Ukombozi bila utii ni safari ya kurudi utumwani.
Baraka bila Neno zinakuwa mfupi.
Neema bila mabadiliko huzaa udini, sio uzima.
Mungu anatuita sio tu kutoka giza, bali kuingia katika nuru (Kol. 1:13). Kuingia katika nuru kunamaanisha kutembea katika Neno, kuacha mienendo ya Babeli, na kukubali kubadilishwa kutoka ndani.
Isaya 55:12–13.
Wapendwa Karibuni -KKKT KARIAKOO -Jumuia kwa Njia ya Zoom.
MADA: IBADA YA JUMUIA
Muda 12:30 ASUBUHI
na Kila Jumamosi,
Join Zoom Meeting/Link ya kujiunga
https://us05web.zoom.us/j/81743899818...
Ama ingiza hizi taarifa baada ya kufungua program yako ya zoom
Meeting ID: 817 4389 9818
Passcode: UP6ymz
Karibuni Mkalete Dhabihu na Matoleo ya Shukrani Nyumbani mwa BWANA 🙏
📖 (2 Nyakati 29:31)
💰 NJIA ZA KUTOA SADAKA:
🔹 M-Pesa: LIPA Namba 📌 5534291
🔹 Tigo/YAS Pesa: LIPA Namba 📌 18333215
🔹 M-Pesa: Namba ya Simu 📞 0766459983
🏦 Maendeleo Bank: Account No. 013795436021
Jina: KKKT Kariakoo
📲 SUBSCRIBE, LIKE & COMMENT kwenye kurasa zetu kwa ajili ya mafundisho zaidi!
📞 Maombi na Ushauri: Wasiliana na Mch. Joash Aila ☎️ 0747444401
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: