TANROADS Songwe yakabiliana na maporomoko ya Udongo unaoziba barabara Ileje
Автор: Gilly Bonny Tv
Загружено: 2023-09-05
Просмотров: 298
TANROADS Songwe yakabiliana na maporomoko ya Udongo unaoziba barabara Ileje
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe unafanya matengenezo ya barabara ya Ibungu- Kalembo – Katengele kwenda - Kafwafwa, Wilayani Ileje, yenye urefu wa kilometa 44 kwa kukata Milima na kuondoa maporomoko ya Udongo ambayo kipindi cha mvua huziba barabara hiyo.
Akizungumza na kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa, toleo maalum la miradi ya Mikoa, Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga amesema matenegezo ya barabara hiyo ambayo inaunganisha mkoa wa Songwe na Mbeya kupitia Wilaya ya Ileje, yanajumuisha kukata milima, kuongeza upana kutoka mita tatu na nusu kwenda mita 10 mpaka mita 12 kisha kujenga kwa kiwango cha zege maeneo yote hatarishi ya barabara hiyo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: