RASMI MANGE KIMAMBI AMEKWISHA, ACCOUNT ZAKE ZAFUNGWA, KESI YA UHUJUMU UCHUMI KUMRUDISHA TANZANIA
Автор: NYOTARAYS TV
Загружено: 2025-12-04
Просмотров: 162
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeahirisha hadi Januari 28, 2026 kesi ya uhujumu uchumi Na. 000021172/2025 inayomkabili Mwanaharakati wa mitandao ya kijamii Mange Kimambi, baada ya upande wa Mashtaka kueleza kuwa upelelezi haujakamilika.
Shauri hilo liliitwa leo, Desemba 4, 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Hassan Makube ambapo upande wa Jamhuri uliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na taratibu za uchunguzi.
Upande wa utetezi haukuwa na wakili mahakamani, jambo lililomfanya Hakimu Makube kuagiza upande wa Mashtaka kuhakikisha upelelezi unakamilika kabla ya tarehe hiyo ili shauri lianze rasmi kusikilizwa.
Mange Kimambi anakabiliwa na shtaka la utakatishaji wa fedha kiasi cha Sh138.5 milioni, akidaiwa kuyapata kati ya Machi 1 na 31, 2022 jijini Dar es Salaam kwa kufanya kazi ya uandishi wa habari bila kibali na kwa kutumia vitisho.
Shtaka hilo linasomeka chini ya kifungu cha 12(1)(d) na 13(a) cha Sheria ya Utakatishaji Fedha (Sura ya 423, 2019) pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi.
Hivi karibuni, video iliyosambaa mitandaoni ilimuonesha Mange akidai kuwa amepata taarifa za kesi hiyo na kudai kuwa Serikali imekusudia kumrudisha nchini kupitia sheria ya usafirishaji watuhumiwa kutoka mataifa ya nje (Extradition Act, 2019).
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, pia amethibitisha kuwa ofisi yake inachunguza uwezekano wa kumchukulia hatua Mange kwa tuhuma za kuchochea maandamano, na kwamba mikataba ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani inatumiwa kufanikisha hilo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: