DC THOMAS AAGIZA WANAOCHOMA MOTO HOVYO WAKAMATWE MARA MOJA LUDEWA.
Автор: LUDEWA ONLINE TV
Загружено: 2025-10-22
Просмотров: 177
DC THOMAS AAGIZA WANAOCHOMA MOTO HOVYO WAKAMATWE MARA MOJA LUDEWA
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Olivanus Thomas, ametoa agizo kwa Jeshi la Polisi, Jeshi la Akiba, pamoja na watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanawafuatilia, kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote wanaochoma moto kiholela wakati wa maandalizi ya mashamba, akisema serikali haitavumilia tena vitendo hivyo vinavyosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na miundombinu.
DC Thomas ametoa maagizo hayo wakati wa semina na uzinduzi wa uuzaji wa majiko bora yanayotumia mkaa kidogo kwa bei ya ruzuku ya serikali, tukio lililoandaliwa na TAWEN kwa kushirikiana na REA na Envotec.
Amesema uchomaji moto holela umefikia kiwango cha hatari, huku akibainisha kuwa wilaya nzima ilikosa huduma ya umeme baada ya moto kuunguza miundombinu ya umeme katika vijiji vya Nindi, Ntumbati, Nkwimbili, Lupingu, Lifuma hadi Makonde.
“Serikali inatumia gharama kubwa kusambaza umeme hadi maeneo ya milimani kama Lifuma na Makonde, halafu mtu mmoja anaharibu kwa moto wa uzembe. Hatuwezi kuendelea kukaa kimya — kila atakayebainika kuchoma moto kiholela atachukuliwa hatua kali,” amesema kwa msisitizo.
Aidha, ameeleza kuwa moto huo umesababisha kukauka kwa vyanzo vya maji na kuungua kwa mashamba ya miti yaliyotunzwa kwa muda mrefu, akisisitiza kuwa tabia hiyo sasa ni tishio jipya kwa mazingira na nishati wilayani humo.
Ameongeza kuwa kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia inalenga kupunguza ukataji wa miti na kulinda mazingira, lakini juhudi hizo hazitakuwa na maana iwapo wananchi wataendelea kuchoma moto ovyo.
“Imetosha! Kuanzia sasa yeyote atakayechoma moto kiholela lazima achukuliwe hatua. Tunataka kuona matokeo, si maelezo,” amesisitiza DC Thomas
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: