SIMANZI! Mwili wa mwigizaji wa Jua Kali 'Kitundu' ukiwasili nyumbani kwao
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-06-26
Просмотров: 34997
Mwili wa aliyekuwa mwigizaji wa Jua Kali, Raidanus Vitalis 'Kitundu' aliyefariki Juni 24, 2025, umewasili nyumbani kwao Vikindu mtaa wa Magomeni ukitokea hospitali ya Temeke ambapo ulikuwa umehifadhiwa.
Mwili huo umewasili nyumbani kwao muda mfupi uliopita, ambapo utaagwa na baada ya hapo utaenda kupumzishwa katika Makaburi ya Wailes, Temeke.
Kitundu alifariki dunia Jumanne jioni, Juni 24, 2025, ambapo taarifa za msiba huo zilitolewa kupitia ukurasa wa Instagram wa mzalishaji na mwongozaji wa tamthilia aliyokuwa akiigiza ya ‘Jua Kali’, Leah Mwendamseka 'Lamata.'
Enzi za uhai wake, Kitundu aliigiza kwenye tamthilia hiyo kama kijana mwenye kipaji cha kucheza muziki anayetokea kwenye familia ya kimasikini. Kisha baadaye anapata nafasi ya kutoboa kimaisha lakini anashindwa kuitumia vizuri na kujikuta akirudi kwenye maisha ya kimasikini.
Lamata alibainisha kuwa kabla ya Kitundu kufariki, alikuwa anaumwa tangu mwaka jana na kupelekea kutoshiriki vizuri kwenye tamthilia ya Jua Kali huku akishindwa kutaja kilichokuwa kinamsumbua zaidi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: