HITIMISHO LA JUMA LA UWAKILI KANISA LA IWAMBI
Автор: Hope Media SHC
Загружено: 2025-06-05
Просмотров: 90
MBEYA
Wito umetolewa kwa washiriki kumtolea Mungu zaka na sadaka kwa mpango ili kuitegemeza kazi ya injili huku wakiendelea kuunga mkono maendeleo ya kanisa mahalia
Mchungaji Solomon Yohana mkurugenzi wa uwakili jimbo la kaskazini mashariki mwa Tanzania ametoa wito huo katika semina za uwakili zilizolenga kuwaelimisha washiriki juu ya njia bora ya kumtolea Mungu zaka na sadaka
Nae mchungaji Charles Mashambo anayesimamia mtaa wa Mbalizi amesema wameamua kuweka juma ilo si kwa sababu hali ya matoleo imeshuka bali ni kuendelea kutoa hamasa ya watu kumtolea Mungu Zaidi
Aidha Kiongozi wa uwakili Emy Samweli amesema masomo yaliyofundishwa kwa juma zima ni ya pekee sana na yataleta badiiko kubwa kijamii kiroho na kiuchumi na kuinua hali ya uchumi na utoaji
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wamekuwa na maoni tofauti juu ya utoaji wa zaka na sadaka huku wengi wakionesha kuwa na uelewa mkubwa wa namna bora inayopaswa kumtolea Mungu
Juma ilo la uamsho la uwakili limefanyika katika kanisa la waadventista wasabato Iwambi likienda sambamba na uzinduzi wa mpango wa ujenzi wa kanisa la kisasa huku likiacha alama kubwa kwani watu wamepata hamasa ya kumtolea Mungu zaka na sadaka kwa mpango na kwa moyo
Na George Muttarogwa
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: