Mtindo wa lugha (Mbinu za lugha na Mbinu za uandishi) katika novela :Mshale wa Matumaini
Автор: Teachkrest International (Ruth K. N)
Загружено: 2024-05-15
Просмотров: 1215
Jazanda
-Mbegu ya uasi
Mkondo wa maji chafu uk 49
Tanakali ya sauti
Baba yangu alitulia tuli
Moyo ulinidunda dududu uk 11
Bak bandika bak bandua uk 16
Choka tiki uk 18 na lala fofofo.
Kataa katakata uk 19
Jasho kutoka chepechepe mwilini ik 20
Jinyoosha twaa uk 22
Tashbihi
Tulia tuli kama maji ya bwawani
Huu ni kama mtego wa panya ushikao waliomo na wasiokuwemo uk 5
Damu zikamwagika kama maji
Sauti ya mama kupasua hewa kama mvua ya kidindia uk 11
Nilitoka nyumbani kama mwizi uk 12
Twaa kama sanamu ya kuchonga uk 22
Zimika ghafla kama kibatari kwenye upepo mkali uk 23
Wacheshi kuvaa sura za huzuni kana waliorushwa kwenye moto wa jehanamu uk 24
Konda kama ngonda uk 25
Nilikuwa kama mgomba wenye mkungu wa ndizi uliokosa nguzo ya kuuhimili. Uk 35
Aliona huzuni iliyoniandama wakati ule mithili ya mfiwa uk 41
Kuzamia vitabu kama mchwa katika ujenzi uk 51
Msako ulikuwa kama neti kubwa baharini uk ,53
Nilitaka wakae kama ndugu wala si kama simba na swara uk 57
Kama mtoto abebwaye mgongoni nilijikaza uk 59
Methali
Lisemwalo lipo na kama halipo lipo njiani laja
Tutahadhari kabla ya hatari uk 5
Kelele za chura hazimuzui tembo kunywa maji uk 7
Lisilo budi hutendwa uk 19
Mhitaji habagui uk 19
Baada ya dhiki ni faraja uk 50
Chendacho mavani hakina marejeo9
Jungu kuu halikosi ukoko
Mtoto wa nyoka ni nyoka uk 42
Nyumbani ni nyumbani ingawa pangoni
Kuinamako ndiko kuinukapo. uk 44
Nidaa
Alaa!
Vita vina hasara, eti!.
Ala! Umerudi tena huu uvumi jamani uk 8
Ghafla niliamka! Dah! Uk 20
Aibu iliyoje! Uk 46
Msemo na nahau
Tuwaonyeshe kilichomtoa kanga manyoya ya shingo
Kutawaka moto- Mambo yatachacha
Akiunga mkono mzozo uliovumishwa- kukubali mzozo
Tumbukia nyongo,- haribika
Ponea kwa tundu la sindano uk 9
Andamana sako kwa bako uk 11
Shika roho mkononi uk
Piga moyo konde uk 17
Nilitoka shoti uk 20- kukimbia
Pata afueni- pona
Piga mbizi katika mawazo- kuogelea tafakari
Takriri.
Hamwezi kutukandamiza miaka nenda miaka rudi- miaka uk 5.
Sikujua nichukue nini niache nini uk 9
Kutana ana kwa ana- Kuonana uso kwa uso uk 35
Kushika tama uk 47
Kufa kupona
Tia kiwewe
Torosha kiguu na njia uk 52
Swali balagha
Lakini nani alijali msongamamano? Uk 16
Ni porojo hizi?
Ni nani anayejua? Uk 48
Ishara
Sauti za njiwa ni sauti za dhiki
Chuku.
Nyayo za Bi. Zulu zina mianya ungedhani ni bonde la ufa uk 15
Utohozi.
Friji- fridge
Plastiki- plastic uk 18
Penalti
Refa uk 19
Kilomita- kilometers
Biblia- Bible
Tashhisi
Upepo kuvuma kwa hasira kubwa uk 16
Maisha yalinionea uk 35-
Hadithi ndani ya hadithi
Kuokolewa kwa Waisraeli
Litifati
Kupachika vifungu kutokana na kitabu, Mshale wa Matumaini
Motifu ya ndoto
Zingo kuota akichezea timu yake ya Nomads
Zingo kuota yu ndegeni kuelekea Uswizi uk 45
Ritifaa
Uk 48. "Nimechoka na hii dunie. Nichukue nije huko nikapumzika na mimi pia. Huwa ninasikia watu huja kupumzika madhila ya dunia
Kinaya
Zingo kutamani nyumbani licha ya kuwa hakukuwa salama uk 47
Ni kinyume cha matarajio kuwa mwalimu wa shule ya msingi anajiunga na wanamgambo
Sadfa
Kutoweka kwa baba na mapigano kuanza
Uvumi wa mlima Gera kulipuka kunasadifu kina Zingo kuwa wakimbizi kule
Kutembelea Mzee Musambale kusadifu habari za vita Doneka katika redio
Deno kutokomea na uvamizi kushamiri
-Zingo kufika hospitalini kunasadifu habari za kifo cha mama MI
Hotuba
Wosia wa mama kwa Zingo akikaribia kufa uk 50
Zingo kuhutubu kuhusu yale yaliyomkaa moyoni uk 58
Dhihaka au stihizai
"Anajifanya msomi sana. Tutaona atafika wapi. Ni duduvule wa vitabu." Uk 51
Kisengere nyuma
Zingo kuangazia maisha yake ya awali ambapo baba alimtembeza nchi nzima kuona vituo vya utalii uk 57
Lakabu
Simba- jina aliloitwa Zingo na mamake alipopendezwa na jambo
Majazi
Zahara- mwerevu, maridadi, kung'aa kama Venus
Zingo
Doneka
Tereka
Gandua
Yenka
Azania
Dayolojia.
Mama na baba
Deno na Zingo
Zingo na Musambale
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: