Semina kwa wanahabari mabalozi wa LATRA
Автор: LatraTV
Загружено: 2025-05-13
Просмотров: 145
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeendesha semina ya kuwajengea uwezo Wanahabari Mabalozi wa LATRA juu ya kazi na majukumu yanayotekelezwa na Mamlaka.
Semina hiyo ya siku mbili imefunguliwa rasmi na CPA Habibu Suluo, Mkurugenzi Mkuu LATRA ambapo katika ufunguzi huo amewapongeza wanahabari hao kwa kuwa mabalozi wazuri katika ufikishaji wa habari zinazohusu sekta ya usafiri ardhini kwa watanzania.
Aidha CPA Suluo amewaasa wanahabari hao kutumia kalamu zao vizuri kuandika habari zinazohusu uchaguzi mkuu na kuepuka habari zinazopotosha jamii pamoja na kuandika kwa umahiri habari zinazohusu sekta ya usafiri nchini.
Semina hii inafanyika ukumbi wa Tari - Kibaha Pwani kuanzia Mei 6 hadi Mei 7, 2025 ambapo mada mbalimbali zinawasilishwa ikiwemo majukumu ya LATRA katika udhibiti usafiri wa reli, Nafasi ya wanahabari katika kutekeleza sheria za LATRA pamoja na Mafanikio ya LATRA katika miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: