MKUU WA WILAYA AHITIMISHA MAKAMBI LUDEWA
Автор: Hope Media SHC
Загружено: 2025-09-02
Просмотров: 61
NJOMBE LUDEWA,
Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe amewataka waumini kutumia vizuri fursa ya mikutano ya makambi ili iwe chachu ya kubadilisha maisha kwa ujumla huku wakiendelea kumtumaini Yesu katika kila Jambo
Mkuu huyo wa wilaya ya Ludewa Mh. Livanius Thomas ameyasema hayo katika hafla ya kuhitimisha mikutano ya makambi mtaa wa Ludewa mkoa wa Njombe ambapo amesisitiza juu ya kuishi na kutimiza matakwa yote yaliyo katika mafundisho yaliyotolewa
Naye mchungaji wa Mtaa wa Ludewa Obadia Mwelela pamoja na mhudumu mkuu wa Kambi ilo mch. Shadrack Mbugi wamesema kambi hilo limekuwa na matokeo makubwa mara baada yakuhitimisha kwa ubatizo na kutoa rai kwa washiriki kuhakikisha wanawalea vyema wale wote waliobatizwa
Akielezea tathimini ya kambi hilo mkuu wa kambi ndugu Obeid Mhagama amesema kumekuwa na mabdiliko makubwa kwani kambi limefanikiwa kwa asilimia 99 na watu wote waliohudhuria wamepatiwa mahitaji ya kiroho pamoja na ya kimwili
Kwa upande wao wale waliobatizwa katika kambi hilo wamesema wanahisi furaha na Amani mara baada yakuingiakatika nurumpya na kwamba wataendelea kuishi kulingana na mafundisho ya neno la Mungu
Kambi la Ludewa limekuwa na matokeo chanya ambayo yameleta mwamko mkubwa wa watu kushiriki katika shughuli za utume kwani katika kuhitimisha washiriki walifanikiwa kuifikia jamii kwa kugawa vitabu vya neno la Mungu
Na George Muttarogwa
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: