WANANCHI WATOA WASIWASI JUU YA MAANDAMANO YA DISEMBA 9...........
Автор: Cawabe Media
Загружено: 2025-11-25
Просмотров: 1059
Wananchi Watoa Wasiwasi Juu ya Maandamano ya Desemba 9, 2025.
Wananchi wa maeneo mbalimbali wameeleza wasiwasi wao juu ya maandamano yanayodaiwa kupangwa kufanyika tarehe 9 Desemba 2025, wakikumbusha athari za matukio ya vurugu yaliyotokea hivi karibuni yaliyoleta uharibifu wa miundombinu na kusababisha kukatiza shughuli za kila siku za wananchi.
Katika mkutano na wakazi wa kata husika, Mkuu wa Wilaya Mhe. Makilagi amewahakikishia wananchi kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama imeimarisha mikakati madhubuti ya kurejesha na kudumisha hali ya utulivu. Aidha, amewataka wananchi kuendelea kulinda amani, kushirikiana na vyombo vya usalama, na kuepuka matendo yoyote yanayoweza kusababisha uvunjifu wa sheria.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: