WATENDAJI WA TUME YA MADINI WATEMBELEA MGODI WA GOD MWANGA
Автор: MOHAB TV ONLINE
Загружено: 2025-10-20
Просмотров: 31
Makamishna wa Tume ya Madini, Mhandisi Theonestina Mwasha na Dkt. Theresia Numbi, wameongoza kikosi cha watendaji wa Tume ya Madini wakiwemo Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa katika ziara ya kutembelea Mgodi wa Madini ya Kinywe (Graphite) wa God Mwanga uliopo wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Ziara hiyo, iliyofanyika Oktoba 17, 2025, imelenga kujionea shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini zinazofanywa na mgodi huo.
Ziara hiyo ni sehemu ya mikakati ya Tume ya Madini ya kufuatilia utekelezaji wa shughuli za madini nchini, kuhakikisha wachimbaji wanazingatia sheria, kanuni na taratibu, pamoja na kuhakikisha usalama wa mazingira katika maeneo ya uchimbaji.
Makamishna wa Tume ya Madini wamesema wamefurahishwa na uwekezaji mkubwa wa kampuni hiyo na kuhimiza Tume ya Madini kuendelea kutangaza fursa za uwekezaji katika madini ya kinywe (graphite), hasa ikizingatiwa kuwa mahitaji ya madini hayo duniani ni makubwa. Aidha, wamesisitiza umuhimu wa kuongeza viwanda vya uchenjuaji wa madini nchini.
KITUO KINACHO JIHUSISHA NA HABARI MBALIMBALI ZA KIJAMII NA KUELIMISHA UMMA KUHUSU MATUKIO YANAYO JIRI KILA WAKATI HAKIKISHA UNA SUBSCRIBE CHANEL YETU USIPITWE NA TUKIO LOLOTE HAPA NCHINI ( Email: [email protected](+255752268249 / +255785537878)
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: