Wamiliki wa timbo waonywa kilifi
Автор: ROYAL ADVANCED NET TV
Загружено: 2025-12-10
Просмотров: 53
Kamati ya kitaifa kuhusu malalamishi ya mazingira imezipatia makataa ya miezi miwili kampuni zinazomiliki timbo kaunti ya Kilifi kuhakikisha zinafuata sheria za uchimbaji madini.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendanji wa kamati hiyo Mary Njogu wamepokea malalamishi kutoka kwa wakazi kuwa wakekezaji katika timbo hizo za kuchimba kokoto na madini zinasababisha uchafuzi wa mazingira unaoathiri wakazi kiafya.
Akizungumza baada ya kutembelea timbo za eneo la Jaribuni eneo bunge la Ganze, Njogu amebainisha kuwa baadhi ya kampuni hazina stakabadhi muhimu kutoka kwa serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya Kilifi ili kutekeleza shughuli zao.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kitengo cha mazingira katika serikali ya kaunti ya Kilifi Jimmy Kahindi amesema watashirikaina na kamati hiyo ya kitaifa ili kuhakikisha wakazi wanaishi katika mazingira yaliyo salama huku akiwataka wawekezaji waonaochimba kokoto wanafuata sheria za mazingira.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: