E’YESU ingia rohoni kabisa (268 NW)
Автор: Shem Kabanza
Загружено: 2020-06-27
Просмотров: 13507
268 #Nyimbozawokovu
268
1. E’ Yesu, ingia rohoni kabisa,
uniweke huru nakunitakasa,
nipate kushirikiana na wewe
katika mateso na raha daima!
Pambio:
:/: E’ Bwana, nijaze
upendo wa mbingu
nao uthabiti,
niwe mshindaji! :/:
2. Siombi ufalme, siombi heshima,
naomba kupewa neema daima,
nijue ukweli wa neno la Mungu:
Mtoe miili na iwe dhabihu!
3. Ingia rohoni, unichungulie,
na katika yote unisaidie,
nipate kabisa kusudi na nia
kujitoa kwako, kukutumikia!
4. Hakuna la huku litanizuia
nisifananishwe na Yesu Masiya.
Nitumainije kufika mbinguni
nisiposhiriki Mwokozi mpendwa!
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: