GGML YAKUMBANA NA CHANGAMOTO YA TEGESHA ULIPAJI FIDIA WANANCHI | SERIKALI YAFIKA GEITA KUTATUA
Автор: Jambo FM Radio Tanzania
Загружено: 2025-11-22
Просмотров: 14
Zoezi la uthamini wa ardhi linalofanywa katika maeneo ya Nyakabale,Manga ,Nyamalembo na Samina mkoani Geita kwa lengo la ulipaji wa fidia kabla wa kutwaliwa na mgodi wa dhahabu wa GGML limefikia asilimia 92.74 sawa na hekari 2790 kati ya hekari 3900 zinazopaswa kufikiwa na zoezi hilo zinazomilikiwa na watu 6053.
Mthamini mkuu wa Serikali, Bi.Eveline Baruti Mgasha amebainisha hayo akiwa mkoani Geita alipofanya ziara yenye lengo la kutatua changamoto zilizotokeza katika zoezi hilo ambazo ni pamoja na aina ya mazao yaliyopandikizwa hivi karibuni kwaajili ya kujipatia fidia maarufu kama tegesha,uwepo wa nyumba zilizoangushwa na mvua za mwezi Septemba mwaka huu.
Mthamini kutoka kampuni ya White Knights Real Estate inayoendesha uthamini huo,Lwitiko Bukuku ameeleza kwamba hatua inayofuata baada ya zoezi la uthamini ni kugawa fomu za kisheria na kuonesha majedwali ya fidia yatakayoonesha stahiki za kila mnufaika kulingana na mali iliyokaguliwa ikifuatiwa na hatua ya kupitishwa na mthamini mkuu kabla ya kupelekwa kwa mlipaji(Mgodi wa GGML) kwaajili ya kuendelea na hatua nyingine za malipo.
Akizungumzia kwa njia ya simu kuhusiana na changamoto ya ‘tegesha’makamu wa rais wa mgodi wa GGML,Bw Simon Shayo amesema mgodi huo utajitahidi kulipa fidia licha ya uwepo wa changamoto hiyo na kutoa wito kwa wananchi kuondokana na tabia hiyo akieleza kwamba fidia si biashara ya faida bali ni mchakato wa kisheria wa kutathmini mali za watu na kuwarudishia pale ambapo malizao na ardhi zao zinapohitajika akibainisha kwamba kufanya mchezo wa tegesha ni kujipotezea muda wa upatikanji wa stahiki zao.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: