Kauli ya Prof Mkenda kuhusishwa na mtuhumiwa wa mauaji ya Beatrice
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2023-12-29
Просмотров: 8911
Mbunge wa Rombo na Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameonyesha kusikitishwa na taarifa zinazosamba mtandaoni za mtu anayedaiwa kumuua Beatrice Minja(47) mkazi wa kijiji cha Mbomai, wilayani humo kuwa ni mfanyakazi wake wa shambani jambo ambalo amesema kijana huyo hamfahamu.
Profesa Mkenda amesema wakati tukio hili linatokea Novemba 12, mwaka huu alishirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi kuhakikisha mtuhumiwa huyo anakamatwa ambaye baada ya kutenda tukio hilo alitoroka kusikojulikana.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, Profesa Mkenda alisema kwa kuwa tukio hilo lilikuwa likichunguzwa na jeshi la polisi asingweza kutoka hadharani na kuzungumza tukio ambalo linachunguzwa na jeshi la polisi ili kutokuharibu upelelezi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: