WANAMTWARA WATAKIWA KUITUNZA AMANI
Автор: HTv Tanzania
Загружено: 2025-03-30
Просмотров: 33
Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwenzi Oktoba mwaka 2025, Wananchi mkoani Mtwara wametakiwa kuendelea kudumisha na kulinda Amani iliyopo huku wakihimizwa kutofumbia macho kwa yeyote mwenye nia ya kuvunja Amani
Hayo yameelezwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanal Patrick Sawala katika tukio la kumuombea dua Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassa lilofanyika katika viwanja vya Mashujaa Pack manispaa ya Mtwara Mikindani, Mh Sawala ametumia nafasi hiyo kuwasihi wananchi kulinda amani na kuacha kushawishika katika uvunjifu wa amani, kwakuwa maendeleo yaliyopo Mtwara yametokana na uwepo wa amani na utulivu.
Awali wakizungumza katika tukio hilo nao viongozi mbalimbali akiwemo Shekhe mkuu wa mkoa wa Mtwara, wameendelea kusisitiza kutunza tunu ya amani sambamba na kuendeleza kufanya matendo mema hata mara baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kwa resma
Dua hiyo pamoja na Iftar imeandaliwa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mtwara kwa kushirikiana na Baraza la waislamu Tanzania Mkoani hapa (BAKWATA)
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: